Mshambuliaji wa AS Roma, Romelu Lukaku ameshutumiwa kwa kuikosea heshima Inter Milan na Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Piero Ausilio baada ya kuondoka San Siro.
Mshambuliaji huyo ambaye aliichezea Inter Milan kwa mkopo msimu uliopita amekiwasha AS Roma na kusababisha uvumi kwamba huenda klabu hiyo kutoka Jiji la Milan linaweza kujaribu kumrudisha.
Hata hivyo, ikumbukwe Inter Milan ilishindwa kutoa kiwango cha pesa ambacho Chelsea ilitaka na wakati mazugumzo yakiendelea, Lukaku alidhaniwa aliwasiliana na Juventus.
Majadiliano kati yake na Juventus yaliaminika kuwa yameizuia Inter Milan lakini Lukaku aliamua kujiunga na kikosi cha Kocha Jose Mourinho baada ya mashabiki kuleta zengwe.
Mashabiki wa Inter Milan walimpokea vibaya Lukaku wakati AS Roma ilipomenyana na timu hiyo kwenye mechi ya Serie A waliposafiri kwenda San Siro mwishoni mwa juma lililopita.
“Sitapenda kuzungumzia mchezaji wa timu nyingine, nataka kufikiria mambo ya sasa sio yaliyopita, Lukaku ameshapita tayari, tulishinda Scudetto pamoja, tulipoteza fainali mbili na alikuwa mchezaji muhimu kwetu.” alisema Piero Ausilio
Tangu alipohamia AS Roma, Lukaku amekuwa na msimu mzuri kwani katika mechi 11 alizocheza amefunga mabao manane katika mashindano yote.
Kuungana na kocha wake wa zamani Mourinho kunaonekana kuzaa matunda kiasi kwamba kuna uwezekano klabu hiyo ikamsajili jumla katika dirisha dogo la usajili Januari.
Hatma ya Lukaku bado ina maswali kwani kocha wa Chelsea, Mauricio Pochettino anamuona kama mchezaji wa ziada.
Lukaku hakusafiri na Chelsea kujiandaa na msimu mpya Marekani, hata hivyo baadhi ya wachezaji waliuzwa kipindi cha kiangazi isipokuwa Lukaku ambaye alitolewa kwa mkopo AS Roma.