Klabu ya Southampton imeendelea kuziweka kapuni ofa zinaendelea kutumwa huko St Mary’s, kwa lengo la kutaka kumng’oa kiungo kutoka nchini Kenya Victor Wanyama.

Katika tarifa za hivi karibuni kumeripotiwa kwamba kati ya nyota wanaowindwa ni pamoja na Sadio Mane na Victor Wanyama.

Tayari klabu za Manchester United, Bayern Munich na Paris St Germain zimeingia katika vita vya kuwawania wachezaji hao ambao ni tegemeo kwa sasa.

Meneja wa Southampton Ronald Koeman alizungumza na waandishi wa habari kuhusu suala hilo na alisema: “Wanazungumzia kuwasajili wachezaji wa Southamton kwa sababu ni wazuri, lakini hakuna kinachoweza kufanyika kwa sasa.”

“Na matamanio ya kila mchezaji ni kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa.”

“Tunajua nini cha kufanya juu ya tunavyoweza kufanya biashara.” “Lakini ukweli ni kwamba, katika dirisha la mwezi Januari hakuna mchezaji atakayehama kutoka Southamton.”

Wanyama mwenye umri wa miaka 24, anatajwa kuingia katika rada za timu za Arsenal na Totenham na kwamba dili la kuondoka lilipangwa kukamilika katika usajili wa majira ya mwezi Januari, mwaka huu.

 

Marouane Fellaini Kuendelea Kusota Old Trafford
Hiddink Bado Ana Matumaini Makubwa Na Chelsea