Hatimae mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Ronaldo de Assis Moreira ‘Ronaldinho’ amekubali kurejea barani Ulaya. Uamuzi wa mchezaji huyo umekuja baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa klabu iliyopanda daraja na kucheza ligi kuu nchini Uturuki, Antalyaspor.

Raisi wa klabu hiyo, Gultekin Gencer, amethibitisha taarifa za kufikia makubaliano chanya na Ronaldinho aliyewahi kutikisa barani Ulaya akiwa na FC Barcelona ya Hispania.

ronaGencer amesema tayari mazungumzo ya awali yameshakamilika na ndani ya juma hili anatarajia kukamilisha mipango ya usajili wa Ronaldinho mwenye umri wa miaka 35, ikiwa ni pamoja na kumsainisha mkataba rasmi wa kuitumikia klabu hiyo.
Tayari klabu ya Antalyaspor imekamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Cameroon, Samuel Eto’o ambaye aliwahi kucheza na Ronaldinho katika kikosi cha Barcelona na kupata mafanikio makubwa. Wawili hao wataungana tena huku matarajio ya mafanikio yakiwa makubwa.
Ronaldinho, amehitimisha mkataba wake wa mwaka mmoja na uongozi wa klabu ya Querétaro ya nchini Mexico, na sasa ni mchezaji huru.

P Square wamuunga mkono Wizkid kususia tuzo za BET
Cech Atishiwa Maisha Baada ya Kujiunga Na Arsenal