Nyota wa Brazil aliyewahi kutamba na klabu za Barcelona, PSG, na AC Milan Ronaldinho Gaucho amesema kuwa anatarajia kustaafu kucheza soka rasmi mwishoni mwa msimu huu ikiwa ni miaka 18 tangu aanze kucheza mchezo huo katika bara la Amerika ya Kusini na Ulaya.

Ronaldinho Gaucho amesema kwa umri wa miaka 36 alionao hivi sasa, anahisi mwili wake unahitaji kupumzika, kwani yeye si kijana wa miaka 26 tena, hivyo hata kasi yake uwanjani imeanza kupungua.

Ronaldinho, mmoja wa wachezaji walioonyesha uwezo wa juu kwa kucheza soka la kuvutia alianza kuwa staa wa dunia mara baada ya kutua FC Barcelona mwaka 2003 ambapo alikuwa sehemu ya mchango wa mabadiliko ya timu hiyo kuwa bora Ulaya na duniani kwa kumla.

“Naangalia nini cha kufanya nimalizie maisha yangu ya soka, plani iliyopo ni kucheza kwa mwaka moja, kisha nitastaafu, nitaelekeza nguvu katika miradi mingine kama muziki,” alisema mchezaji huyo.

Zanzibar Queens Yaendelea Kuwa Mdebwedo
Wahitimu Wa Vyuo Vya Ufundi Stadi VETA Waiomba Serikali Kuwapatia Ajira