Mshambuliaji hatari na mfungaji bora wa muda wote wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, amelianzisha kwa kusema yeye na mastaa kadhaa wanaweza kuondoka Santiago Bernabeu.

Ronaldo amemwambia rais wa Madrid, Florentino Perez kuwa hawataweza kuendelea kuvumilia matusi na zomea zomea ya mashabiki wao.

Alisema hivi sasa wachezaji hawana amani kwenye dimba la Bernabeu kwani mashabiki wamekuwa wakitaka ushindi kwa kila mechi, kinyume na hivyo ni matusi na vitisho kwa wachezaji.

“Sidhani kama inafaa kwa mashabiki kuwatukana na kuwatisha wachezaji baada ya kupoteza mchezo mmoja kati ya mechi 20, ni kitu kisichokubalika,” alisema Ronaldo.

Wachezaji wa Real Madrid walikuwa na wakati mgumu walipokubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa mahasimu wao, Barcelona.

Licha ya kuungwa mkono na rais wao, Florentino Perez, wachezaji na hata kocha wao Rafael Benitez, wanaonekana kutokuwa na amani moyoni. .

Ronaldo alihitimisha kwa kusema kuwa, inaumiza sana kuona mashabiki ambao wamekuwa wakiwashangilia kila wanaposhinda, leo wamegeuka na kuwatukana kwa kupoteza mchezo mmoja.

Licha ya malalamiko hayo, Ronaldo ameendelea kuwa mwiba kwa timu pinzani kwa kupachika mabao na jana usiku alifunga mara mbili katika mchezo wa La Liga dhidi ya Real Sociedad  katika ushindi wa 3-1.

Sir Alex Ferguson Kurejea Man Utd
Bojan Kuwindwa Kwa Udi Na Uvumba Januari 2016