Mshambuliaji kutoka nchini Ureno, Cristiano Ronaldo ameendelea kudhihirisha ubora wake katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, baada ya kuisaidia klabu yake ya Real Madrid kupata ushindi katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi dhidi ya mabingwa wa soka kutoka nchini Ukraine, Shakhtar Donetsk.

Ronaldo, alilazimika kusubiri hadi mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa, Karim Benzema alipofunga bao la kuiongoza Real Madrid, katika mchezo huo na ndipo alipofanikisha ufungaji wa mabao mengine matatu kupitia mguu wake.

Hata hivyo mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa na Ronaldo, yalitokana na mikwaju ya Penati ambazo zilisababishwa na uzembe uliokua ukifanywa na safu ya ulinzi ya Shakhtar Donetsk hali ambayo ilipelekea beki Taras Stepanenko kuonyeshwa kadi nyekundu.

Hata hivyo mchezo huo haukumalizika salama kwa Real Madrid, kutokana na mshambuliaji wao kutoka nchini Wales Gareth Bale kuumia kiazi cha mguu katika dakika ya 28 na alilazimika kutolewa nje.

Meneja wa klabu ya Real Madrid, Rafael Benitez amesema kuumia kwa Gareth Bale ni pigo kubwa sana kwake, lakini hatochoka kuhakikisha mambo yanamuendelea vizuri kama alivyojipanga tangu mwanzoni mwa msimu huu.

Amesema Bale ni mchezaji muhimu katika kikosi chake na hana budi kukubaliana na hali halisi iliyojitokeza katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo lakini akasisitiza ataendelea kumuombea mungu ili aweze kurejea mapema uwanjani.

Matokeo ya michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundu iliyochezwa jana kwa ujumla.

Champions League – Group A

Paris Saint Germain 2 – 0 Malmo FF
Real Madrid 4 – 0 Shakhtar Donetsk

Champions League – Group B

PSV Eindhoven 2 – 1 Manchester United
Wolfsburg 1 – 0 CSKA Moscow

Champions League – Group C

Benfica 2 – 0 FC Astana
Galatasaray 0 – 2 Atletico Madrid

Champions League – Group D

Manchester City 1 – 2 Juventus

Sevilla 3 – 0 Borussia Moenchengladbach

Godbless Lema Amgeukia Wema Sepetu
Man Utd Wapata Pigo Kubwa Ugenini