Uwezekano wa nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro kurejea Manchester United unaendelea kudhihiri, kwa mujibu wa taarifa zilizopo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 huenda akaondoka kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa zinaeneleza kuwa Juventus FC wanatarajiwa kumtoa mshambuliaji huyo kabla ya kumaliza mkataba wake wa sasa unaomalizika 2022 na kutaka kukimbia mshahara wa Pauni 850,000 wanaomlipa kwa juma.

Hata hivyo taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la Madrid la AS zinaeleza kuwa, Ronaldo hana mpango wa kundoka mwishoni mwa msimu huu kama inavyoelezwa, na huenda akasubiri hadi kuwa mchezaji huru mwaka 2022.

Taarifa pia zilidai kuwa Juventus pia ina furaha kuendelea kubaki na mchezaji huyo hadi mwisho wa mkataba wake, endapo hawatatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Hata hivyo, Man Utd inaweza kutaka kumsajili kabla ya Ronaldo kufikisha umri wa miaka 37.

Vyombo vya habari vya Ureno vimeandika kuwa maofisa wa klabu hiyo ya Old Trafford wameshaanza mawasiliano na wakala wa Ronaldo kwa nia ya kutaka kumsajili tena.

Ronaldo anaweza kushawishika kukatisha mkataba wake kuendelea kuitumikia miamba hiyo ya Turin, kutokana na Lionel Messi.

Nyota huyo wa Barcelona na hasimu wa muda mrefu wa Ronaldo anajiandaa kuondoka Hispania kama mchezaji huru 2021.

Na anatarajiwa kujiunga na Manchester City kuendeleza uhusiano mzuri alionao na meneja Pep Guardiola.

Jafo aahidi makubwa endapo atateuliwa
Karia awaomba watanzania, CAF yaanika waamuzi