Cristiano Ronaldo amekiri kuwa anatamani angekuwa na mguu wa kushoto wa mpinzani wake Lionel Messi aliyeshinda tuzo ya Ballon d’Or 2015 kwa mara ya tano na kuvunja rekodi.

Kwa mujibu wa Mirror, Ronaldo aliyasema hayo jana baada ya kutolewa kwa tuzo hiyo. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid ameitoa kauli hiyo ikiifunika kauli yake ya awali kuwa anaamini bado yeye ndiye mchezaji bora zaidi wa mpira wa miguu duniani.

“Nini ninachotamani kutoka kwa Messi? Mguu wake wa kushoto ni mzuri sana, ningependa kuwa nao,” alisema Ronaldo kabla ya Neymar kuingilia na kudai yeye angependa kuwa na miguu yote miwili ya Messi.

Uhusiano kati ya Messi na Ronaldo ulionekana kuongezeka kabla ya tuzo hizo jana kuliko wakati mwingine wowote. Ronaldo alitegemea matokeo hayo mwaka huu.

UVCCM wataka CCM imfukuze Amani Karume
CCM wamjibu Maalim Seif, Watahadharisha 'nguvu ya umma'