Cristiano Ronaldo amemcharukia kocha wake Rafa Benitez baada ya kukataa moja ya magoli yake wakati wa mazoezi ya klabu hiyo .

Ronaldo alinaswa na camera juzi akitupa mikono na kutamka neno ‘Vai Caralho!’ kuashiria kukasirishwa na tukio hilo lililofanywa na kocha wake.

Kwa lugha ya kireno, mtu hutamka neno hilo akioneshwa kukasirishwa na maamuzi fulani, maana yake halisi ni “unapenda kufanya kila kitu kinyume na Wareno”.

Baada ya hapo tena aliongea maneno ya kejeli dhidi ya mchezaji mwenzake Alvaro Arbeloa wakati walipoewa zoezi la kugongesha mwamba lakini yeye akasema, “Tunatakiwa kutumbukiza mpira wavuni na sio upuuzi huu”.

Uhusiano wa Ronaldo na Benitez unaarifiwa kuwa na walakini hasa mara baada ya hivi karibuni Benitez kuulizwa nani anadhani ni mchezaji bora wa dunia, lakini Benitez aligoma kumtaja Ronaldo na badala yake kumfananisha na wachezaji wengine tu.

Wenger Awaahidi Makubwa Mashabiki Wa Arsenal
Bayern Munich Wakamilisha Yao Kwa Vidal