Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameondoka kwa hasira katika katika chumba cha mahojiano baada ya mwandishi aliyekuwa anafanya nae mahojiano kuulizwa swali juu ya rekodi ya ufungaji magoli katika mechi za ugenini msimu huu.

Ronaldo mwenye miaka 31, amefunga magoli 32 msimu huu lakini hajafunga nje tangu mwezi Novemba.

“Nani mwingine amefunga magoli mengi ugenini kuliko mimi tangu nimekuja Hispania? Aliuliza Ronaldo mfungaji namba moja wa Championzi Ligi”Taja mchezaji mmoja ambaye amefunga kuliko mimi. Hakuna jibu? Sawa. Asante” Akaondoka.

Ronaldo alikuwa akiongea na wanahabari kabla ya mechi ya Jumatano ya Real Madrid dhidi ya Roma katika Stadio Olimpico Mwezi Disemba, mreno huyo alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 10 katika mchuano wa makundi,Goli lake la 11 ni la ugenini lakini hajafunga katika mechi nne za ugenini.

Mayanja: Naujua Udhaifu Wa Yanga
Amis Tambwe Atupa Dongo Mtaa Wa Msimbazi