Mshambuliaji wa Klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo anakabiliwa na mashtaka mbele ya Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA), kwa ushangiliaji wa goli lake la tatu dhidi ya Atletico Madrid, usiozingatia maadili ya soka.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, alibipu rungu la UEFA baada ya kumuiga Bosi wa Atletico, Diego Simeone kwa lengo la kulipiza kisasi lakini aliifanya kwa namna yake pia.

Katika mchezo wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa, Semeone aliwageukia mashabiki na kushika sehemu zake za siri wakati timu yake ilipojipatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Juventus.

EUFA ilimuadhibu vikali Semeone baada ya kujiridhisha kuwa hakuzingatia maadili na kwamba alifanya kwa makusudi, hivyo aliamuriwa kulipa faini ya £17,000.

Shirikisho hilo la Soka linatarajia kutoa uamuzi wake dhidi ya Ronaldo, Machi 21 mwaka huu lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa hautahusu kumfungia.

Ronaldo aling’aa kwenye mchezo kati ya mafahari hao akilipa kisasi kwa nguvu na kupachika magoli yote matatu na kuandika matokeo ya 3-0, Jumanne ya juma lililopita.

 

Maalim Seif afunguka kwanini hakwenda Chadema, alivyoteta na ACT-Wazalendo
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 19, 2019