Mshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo ana matumaini ya kusitisha mpango wake wa kustaafu na kuendeleza maisha yake ya soka ili kushiriki Kombe la Dunia mwaka 2026.

Cristiano Ronaldo amebadili mpango wa kustaafu huku akikataa kumuacha kwenye ushindani mpinzani wake, wa Lionel Messi.

Ronaldo anayekipiga Klabu ya AI Nassr ya Saudi Arabia inadaiwa amewaambia mabosi wake hao yuko tayari kuongeza mkataba mwingine kwani hana mpango wa kustaafu kwa sasa.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ureno, anataka kuendelea kucheza hadi atapofikisba miaka 40 na bado ana matumaini ya kucheza Kombe lijalo la Dunia mwaka akiwa na taifa lake na pengine baada ya hapo atatundika daruga.

Hapo awali Ronaldo alidai kuwa alitaka maisha yake ya soka walau yasizidi mwaka 2024 ambayo yatajumuisha fainali za Euro msimu ujao wa joto, hata hivyo anataka kusalia kucheza hadi 2027.

Ronaldo atasherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 39 Februari mwakani, na atakapokuwa anacheza Kombe la Dunia atakuwa na miaka 41.

Che Malone: Al Ahly ni wagumu, watafia Dar
Mwakalebela awapa somo Viongozi, Kocha Young Africans