Mshambuliaji kiungo nyota wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2017. (Ballon d’Or) ambayo hutolewa na (FFF).

Ambapo nyota wa Barcelona Lionel Messi ameshika nafasi ya pili, huku mchezaji nyota wa Paris Saint-Germain Neymar Jr akishika nafasi ya tatu. Nafasi ya nne imeshikiliwa na golikipa mkongwe wa Juventus Gianluigi Buffon. Nafasi ya tano imeenda kwa Luka Modric, sita ni Sergio Ramos na saba ni Klylian Mbappe.

“Nina furaha ndani ya Real Madrid na ninawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano wanaonipa hadi kupata mafanikio haya, nina imani nitamaliza maisha yangu ya soka ndani ya Real Madrid”, amesema Ronaldo.

Cristiano Ronaldo anashinda tuzo hiyo kwa mara ya tano na kuwa sawa na mpinzani wake wa karibu nyota wa Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye ameshatwaa tuzo hiyo mara tano.

Kinyang’anyiro hicho cha kusaka tuzo hiyo kiliwahusisha wachezaji 30 waliong’aa kwenye soka la duniani kwa mwaka 2017 ambao walitangazwa Oktoba 9 kabla ya mshindi ambaye ni Ronaldo kutangazwa usiku wa jana kwenye sherehe zilizofanyika jijini Paris Ufaransa.

 

 

Lema akanusha kupigana, azidi kumtabiria Mnyika
Breaking News: Anna Mghwira atangaza kujiunga CCM