Nahodha na Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro, ametimiza ndoto za kufikisha zaidi ya mabao 100, akiwa na jezi ya timu ya taifa lake.

Ronaldo alitimiza ndoto hiyo usiku wa kuamkia leo, wakati wa mchezo wa UEFA National League dhidi ya Sweden.

Katika mchezo huo, Mshambuliaji huyo wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC alifanikiwa kuifungia timu yake mabao mawili, yaliyoipa ushindi Ureno.

Kwa hatua hiyo Ronaldo amefiksha mabao 101 akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Ureno, na anakua mchezaji pekee wa taifa hilo kuwa na idadi kubwa ya mabao kwa upande wa timu ya taifa.

Anakuwa mfungaji bora wa muda wote katika timu ya taifa ya Portugal akifuatiwa na Pauleta (47), Eusebio (41), Luis Figo (32) na Nuno Gomes (29).

Ronaldo amekuwa na muendelezo mzuri katika timu yake ya taifa baada ya kukosa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Croatia waliofanikiwa kushinda mabao manne kwa moja.

Kwa upande wa mpinzani wake katika sola la dunia Lionel Messi, Ronaldo anaendelea kuwa juu kwa kufikisha idadi kubwa ya mabao, hukua kimuacha mwenzake kwa tofauti ya mabao 31.

NEC yatoa maamuzi ya rufaa 34 za ubunge, 13 ndani ya kinyang'anyiro
Watanzania msisafiri bila vibali - RC Mtwara