Aliyekuwa mshambuliaji harati wa timu ya taifa ya Brazil, Ronaldo de Lima amemfagilia straika wa Barceona, Lionel Messi kwa kusema kwamba ni mchezaji ambaye amekamilika kwa kila kitu kuliko Cristiano Ronaldo.

Vinara hao wawili kwa sasa wanachuana wakiwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or ambayo wamekuwa wakipokezana kwa ipindi cha miaka saba iliyopita.

Katika kipindi hicho, Messi ameweza kuitwaa mara nne wakati staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameibeba mara tatu ikiwemo ya mwaka 2013 na 2014.

Ronaldo de Lima (pichani kushoto) ambaye naye amewahi kutwaa tuzo hiyo, alisema kuwa Muargentina Messi ndiye anayepaswa kuchukua tuzo hiyo kwa mwaka huu. “Namchagua Messi,” staa huyo wa zamani aliuambia mtandao wa Clarin.

“Naona Messi ndiye aliyekamilika kuliko Ronaldo.”

Mwinyi Haji Ngwali Afurahishwa Na Mapinduzi Cup
Nyundo Ya Magufuli Kuwashukia Wanaotoa Mimba