Majina ya wanaowania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu yamewekwa hadharani na kuna nyota kadhaa wa Ligi Kuu England waliojumuishwa kwenye orodha hiyo.
Nyota kama Erling Haaland, Kylian Mbappe na Lionel Messi wote walijumuishwa kwenye orodha ya tuzo hiyo lakini gwiji na staa wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo akikosekana tena.
Messi alirejea kwa mara ya kwanza kwenye uteuzi kufuatia kuachwa kwenye orodha ya wachezaji 30 walioteuliwa kuwania tuzo ya 2022, Hata hivyo, wakati huu, Messi atazamiwa kuwa miongoni mwa watu wanawaoweza kubeba tuzo hiyo na kuwa ya nane kwake.
Messi, baada ya kunyakua taji la Ligue1 akiwa na PSG na Kombe la Dunia akiwa na Argentina Desemba mwaka, anapewa kipaumbele kuwa anaweza kuwa mshindi.
Hata hivyo, Messi anatazanmiwa kupata ushindani mkubwa kutoka kwa nyota wa Manchester City, Haaland ambaye alikuwa na msimu mzuri na timu hiyo akibeba mataji matatu likiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA, Premier na FA.
Haaland na wachezaji wenzake sita wa City wapo kwenye orodha ya walioteuliwa kuwania Ballon d’or ambao ni Kevin de Bruyne, Rodri, Ruben Dias, Julian Alvarez, Josko Gvardiol na Bernardo Silva. Mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa Oktoba 30.