Mshambuliaji wa klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia Cristiano Ronaldo anakabiliwa na kesi ya kujibu yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.
Kesi hiyo iliyowasilishwa katika Mahakama ya Wilaya huko Florida, nchini Marekani, inadaiwa CR7 anatuhumiwa kwa kutangaza biashara ya ubadilishanaji wa sarafu ya kidijitali (Crypto Exchange Binance).
Kesi hiyo imewasilishwa mahakamani Novemba 27, Ronaldo akituhumiwa kwa kutangaza dhamana ambazo hazijasajiliwa na kujihusisha na udanganyifu kwa kushirikiana na Binance.
Walalamikaji, Michael Sizemore, Mikey Vongdara na Gordon Lewis, wamesema wamepata hasara kutokana na uhamasishaji wa Ronaldo na wanataka kulipwa fidia ya kiasi kinachozidi dola bilioni 1.
Shida hii ya kishernia inatokana na ushirikiano wa miaka mingi wa Ronaldo na Binance, walioingia katikati ya mwaka 2022 ili kutangaza sarafu hizo maarufu kama NFTs (non-fungible tokens).
BBC imewasiliana na kampuni ya usimamizi ya Ronaldo na Binance ili kusikia maoni yao lakini hawana tamko wala maoni yoyote kutoka kwenye timu ya Ronaldo na wanasheria wake.