Nahodha na mashambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo usiku wa kuamkia hii leo alifunga bao lake la 500 tangu alipoanza kucheza soka mwaka 1992.

Ronaldo, alifikisha idadi ya mabao 500 katika mchezo wa mzunguuko wa pili wa hatua ya makundi wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, ambapo Real Madrid walipambana na mabingwa wa soka nchini Sweden, Malmo FF.

Katika mchezo huo, Ronaldo alifunga mabao mawili yaliyoipa ushindi Real Madrid na kuendelea kuwaweka kileleni mwa msimamo wa kundi A ambalo linajumuisha timu nyingine za Shakhtar Donetsk pamoja na Paris Saint Germain.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30, alitarajiwa kufikisha idadi ya mabao 500 na zaidi mwishoni mwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ligi ya nchini Hispania lakini mambo yalikuwa magumu kwa Real Madrid baada ya kulazimishwa matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Malaga.

Kwa upande wa klabu ya Real Madrid, Ronaldo ameifikia rekodi iliyokua imewekwa na aliyekua nahodha na mshambuliaji wa klabu hiyo Raul Gonzales ya kufunga mabao 323.

Abiria 900 Waliokwama Na Treni Dar Wapaza Sauti
Van Gaal Awasihi Wachezaji Wa Man Utd