Klabu ya Juventus inaendelea kusubiri maamuzi ya Mshambuliaji Cristiano Ronaldo (36), kuhusu hatima yake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Italia.

Juventus inaendelea kufanya subra hiyo, baada ya kikosi cha Ureno kutupwa nje ya fainali za UEFA Euro 2020, kwakufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Ubelgiji mwanzoni mwa juma hili.

Taarifa kutoka mjini Turin zinaeleza kuwa Ronaldo yupo kwenye rada za miamba Manchester United na Paris Saint-Germain dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Tuttosport wameripoti Ronaldo atalazimika kuwaambia Juventus kama anataka kubaki au kuondoka kwenye timu hiyo katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Licha ya umri wake mkubwa, Ronaldo bado anaendelea kuonyesha makali yake ndani ya uwanja, ambali alifunga mabao 36 katika mechi 44 alizocheza msimu uliopita.

Ronaldo amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kwenye kikosi hicho cha Turin.

KMC FC kuikabili Simba SC kwa Mkapa
Sancho kutua Old Trafford