Mshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo amesema ushindani wake na Lionel Messi “umetoweka,” na tayari “tumebadilisha historia ya soka.”

Wawili hao wametawala mchezo huo kwa zaidi ya muongo mmoja, wakishinda mataji 79 kwa pamoja na kuwa wachezaji wawili pekee waliofunga zaidi ya mabao 800 kila mmoja.

“Sioni mambo kama hayo, ushindani umekwisha,” amesema Ronaldo katika mahojiano na ESPN.

“Ulikuwa mzuri, watazamaji walipenda. Wanaompenda Cristiano Ronaldo sio lazima wamchukie Messi na kinyume chake, tumefanya vizuri, tumebadilisha historia ya soka. Tunaheshimika duniani kote, hilo ndilo jambo muhimu zaidi.

“Amefuata njia yake na mimi nimefuata yangu, bila kujali kucheza nje ya Ulaya. Kwa nilivyoona, amelkuwa akifanya vizuri na mimi pia. Urithi unaendelea, lakini sioni ushindani kama huo.

Tulishiriki jukwaa mara nyingi, ilikuwa miaka 15. Sisemi sisi ni marafiki, sijawahi kula naye chakula cha jioni, lakini sisini wafanyakazi wenzake kitaaluma na tunaheshimiana.”

Mshindi wa Kombe la Dunia Messi alijiunga na Inter Miami CF Juni kamna mchezaji huru baada ya misimu miwili katika klabu ya Paris Saint-Germain.

Nahodha wa Argentina Messi ndiye mchezaji wa soka aliye pambwa zaidi aliposhinda kombe lake la 44 baada ya kuisaidia lnter Miami kubeba Kombe la Ligi 2023 Agosti.

Ronaldo, wakati huo huo, alishinda taji lake la kwanza akiwa na Al-Nassr ya Saudi Pro League, klabu ambayo alijiunga nayo Januari kutoka Manchester United, aliponyanyua Kombe la Ligi ya mabingwa ya Kiarabu mwezi uliopita.

Nahodha huyo wa Ureno amekuwa mchezaji pekee kufunga mabao 850 katika historia kufuatia kufunga kwenye ushindi wa 5-1 Jumamosi dhidi ya Al Hazem.

“Ni alama ya kihistoria,” aliongeza Ronaldo mwenye umri wa miaka 38.

“Kwangu ilikuwa ni fahari kwa idadi niliyopata, ambayo sikufikiri ningeweza kufikia.

“Lakini nataka zaidi. Wakati wa kucheza mchezo.”

Mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or pia anajivunia kuwa mwanzilishi wa wachezaji wengine nyota waliojiunga na Saudi Pro League.

Mwanzoni mwa majira ya joto, Karim Benzema na N’Golo Kanté walijiunga na mabingwa watetezi wa Saudi Pro League Al Ittihad.

mlinda mlango wa Senegal Édouard Mendy alisajiliwa Al Ahli, na nyota wa zamani wa Chelsea Kalidou Koulibaly alijiunga na Al Hilal.

Zaidi ya hayo, Marcelo Brozovic alihamia AlNassr ya Ronaldo, Roberto Firmino alikamilisha uhamisho wa bila malipo kwenda Al Ahli baada ya kuondoka Liverpool, na nyota wa Brazil Neymar akasajiliwa Al Hilal kufuatia uhamisho wa euro milioni 90 kutoka PSG.

Kocha Azam FC amkingia kifua Alassane Diao
KITAIFA: Serikali kubuni programu tumizi utambuzi risiti halali