Ronda Rousey ambaye alikuwa mwanamke bingwa wa UFC,  mchezo wa ngumi na mateke ‘asiyepigika’ , kabla ya kujikuta akidundwa vibaya na Holly Holm, ameelezea maumivu makali aliyoyapata kutokana na kipigo hicho.

Rousey ameliambia jarida la ESPN kuwa kipigo alichokipata usoni kimesababisha meno yake kulegea na kwamba meno yake hayajapata nguvu za kutosha hata kutafuta tunda laini aina ya ‘apple’.

Ronda akipokea Kipigo cha Holm

Ronda akipokea Kipigo cha Holm

Alisema kwa namna anavyojisikia, inaweza kumchukua hadi miezi sita.

“It might be three to six months before I can eat an apple, let alone take an impact,” alisema Rousey.

Taarifa zinaeleza kuwa Rousey amelazimika kufanyiwa upasuaji ili aweze kurekebisha mdomo wake uliopasuliwa na teke la Holly Holm.

Hata hivyo, Rousey hajakubali kilichomtokea kwa kupigwa vibaya na Holly Holm na ameamua kurudiana naye ikiwa ni hatua za kutaka kurejesha ubingwa wake.

Kendrick Lamar Afunika Tuzo Za Grammy 2016, Aongoza Kutajwa
Waliokwepa Kodi Wajisalimisha, Walipa Mabilioni, Majina Yao Yako Hapa