Baada ya kipindi kirefu cha mabishano ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wakitaka kuwepo mechi ya marudiano kati ya mwanamke aliyekuwa bingwa wa dunia wa mapigano ya ngumi na mateke (Bantamweight championship, UFC), Ronda Rousey na aliyemnyang’anya taji hilo Holly Holm, hatimaye majibu yamepatikana.

Rais wa UFC, Dana White alithibitisha kuwepo kwa pambano la marudiano kati ya wababe hao alipokuwa akifanya mahojiano na ESPN.

“Ndio, pambano hilo litakuwepo. Sijajua ni lini lakini pambano hilo lazima litakuwepo,” alisema Dana White na kuongeza kuwa wababe hao wamekubali kufanya pambano la marudiano.

Katika hatua nyingine, Rousey anatarajiwa kuwa nyota wa filamu mpya ‘Roadhouse’.

ISIS Watoa Vitisho Vipya Kwa Urusi Na Marekani, Watuma Video Wakimchinja Mpelelezi Wa Urusi
Mahakama Kuu Yamtaka Kafulila Kulipa Milioni 7.5