Kuelekea katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza utakaozikutanisha Machester United na Everton kocha wa Man Utd Jose Mourinho amesema mshambuliaji Wyne Rooney ambaye kwa sasa anaichezea Everton atapata heshima anayostahili.

Mourinho ameyasema hayo akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuelekea katika mchezo utakaozikutanisha Man Utd na Everton siku ya Jumapili katika dimba la Old Trafford.

Rooney ambaye amesajiliwa na Everton msimuu huu atakuwa akirejea katika uwanja wa Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu aachane na Man Utd mapema mwezi Julai.

Mshambuliaji huyo anayeshikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Man Utd alirejea katika klabu yake ya utotoni ya Everton baada ya kuondoka katika klabu hiyo kwa maiaka 13.

Rooney mwenye umri wa miaka 31 aliichezea Manchester United michezo 559 na kufanikawa kufunga jumla ya mabao  253.

Wakati Rooney akirejea katika dimba la Old Tafford mshambuliaji Romelu Lukaku naye atacheza dhidi ya klabu yake ya zamani ya Everton kwa mara ya kwanza tangu alipoondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Manchester United.

Kikongwe wa miaka 117 afariki dunia
Korea Kaskazini yatoboa siri dhidi ya mpango wake wa nyuklia