Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema rais wa Marekani ni adui mkuu wa taifa hilo kuanzia utosini hadi kwenye unyayo.

Ameyasema hayo wakati akijibu ujumbe wa rais Trump alioutoa kupitia ukurasa wake wa twitter

Katika ujumbe wake rais Trump amesema kuwa waandamanaji wa Iran wanadai haki yao ambayo wamekuwa wakipigania kwa miaka mingi kuhusu njaa na kukosekana kwa uhuru wao.

Aidha, picha zimeonyesha waandamanaji wakikabiliana na Polisi katika maandmano yaliyoanza tangu siku ya alhamis ambayo yanaendelea kusambaa katika miji mingine nchini humo.

Hata hivyo, Polisi mmoja ameuawa na waandamanaji hao ambao baadhi yao wanajihami kwa bunduki aina ya rifle na hivyo kufanya idadi ya watu 13 kuuawa hadi sasa.

 

 

Mateka 700 wafanikiwa kutoroka
Magazeti ya Tanzania leo Januari 2, 2018