Boniface Gideon – TANGA.

Utepe wa michauano Kombe la ulinzi Cup umekatwa rasmi katika dimba la Magomeni ambapo timu za Magomeni Star na Edo Combine kutoka Mwakidila, zilikutana na mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya Penati 4-2 baada ya dakika 90 kumalizika kwa milango ya timu zote mbili kuwa migumu.

Michuano hiyo, iliyoandaliwa na kudhaminiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga itazikutanisha timu 20 kutoka katika mitaa mbalimbali ya jiji la Tanga, ikiwa na lengo la kuhamasisha Vijana kuachana na matumizi ya Dawa za kulevya.

Akizindua michano hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe alisema michezo kwa sasa ni furaha na ajira lakini lengo lao hasa ni kipenyeza ujumbe kwa jamii kupiga vita matumizi ya Dawa za kulevya.

Aidha, alisema sambamba na ujumbe wa michauano hiyo kwa mwaka huu bado jeshi hilo linaendelea kusisitiza usalama wa maisha ya watu na mali zao, hivyo kuwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.

Michuano hiyo, itakayozihusisha timu 20 itachezwa kwa mfumo wa mtoano mpaka bingwa atakapopatikana, huku zawadi mbalimbali zikiwa zinazidi kuvutia timu kuzidi kujipanga zaidi.

Azam FC yafafanua usajili wa Alassane Diao
FIFA yaiondolea vikwazo Zimbabwe