Mkali wa ‘Yule’, huenda angekuwa mmoja kati ya wachezaji wakubwa wa mpira wa miguu ambao wangekufanya uhudhurie Uwanja wa Taifa kuona Skillz zao.

Ruby ameeleza kuwa kabla ya kujikita katika uimbaji, aligundua kipaji chake cha kucheza mpira wa miguu na kukifanyia kazi kwa kiwango cha juu.

Akiongea na Lil Ommy kwenye The Playlist ya 100.5 Times Fm, Ruby alisema kuwa aliweza kucheza mpira kwa kiwango cha kitaifa hadi kuingia katika timu ya watoto ya Taifa ya mpira wa miguu wanaoandaliwa, Young Twiga Stars.

“Ningekuwa mcheza mpira wa miguu. Nilikuwa nacheza mpira wa miguu, I swear… namba nane. Nilikuwa kwenye Young Twiga Stars. Yaani nilikuwa napenda sana mpira na mpaka kesho napenda sana mpira wa miguu na naweza kucheza hata nikiingia uwanjani,” Ruby aliiambia The Playlist ya 100.5 Times Fm.

Mbali na kipaji cha kusakata kabumbu, mrembo huyo ameeleza kuwa alikuwa na kipaji cha ubunifu wa mitindo ya mavazi na alianza kukifanyia kazi kwa nguvu hata kabla ya kuingia kwenye muziki.

“Mimi kabla ya kuwa mwimbaji, wazazi wangu walijua nitakuwa designer, kwa sababu I used kufanya vitu vingi sana ambavyo vinastick kwenye upande wa kudesign.”

Lowassa Asema Anajipanga Upya, Ukawa Kuhamishia Kambi Zanzibar
Samsung Yamwagia Rihanna Mabilioni Kwa Mchongo Huu