Rufaa ya klabu ya Real Madrid ya kupinga kuenguliwa katika michuano ya Kombe la Mfalme kwa kuchezesha mchezaji asiyeruhusiwa imegonga mwamba. 

Mabingwa hao mara 19 wa michuano hiyo walienguliwa kwa kumchezesha winga Denis Cheryshev katika mchezo dhidi ya Cadiz uliochezwa Desemba 2 mwaka huu. 

Cheryshev alipaswa kutumikia adhabu yake kutocheza mechi moja ambayo aliipata wakati akicheza kwa mkopo Villarreal msimu uliopita. Mahakama ya Michezo ya Hispania ilitupilia rufani ya Madrid baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote kuhusiana na sakata hilo. 

Madrid kwasasa wanashikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa La Liga nyuma ya mahasimu wao Barcelona na Atletico Madrid.

Pep Guardiola Amekuja Kupumzika Afrika
Ufisadi wa Mabilioni waibuliwa tena Bandarini, Maelfu ya Makontena Na Magari Yavushwa