Shirikisho la soka nchini TFF, limepokea rufaa kutoka Klabu ya Polisi Dar es Salaam dhidi ya Klabu ya Simba kuhusu kumchezesha Mchezaji Novalty Lufunga katika mchezo wao wa Raundi ya Tano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup 2017.

Madai ya Polisi ni kwamba Mchezaji Novalty Lufunga alioneshwa kadi nyekundu kwenye Simba dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup 2015/2016 uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Januari 22, mwaka huu.

Shirikisho hilo limetupilia mbali rufaa hiyo kwa kukosa vigezo vya kikanuni katika uwasilishaji wake na hivyo kukosa sifa ya kusikilizwa. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 18 (1) na (2) ya Kanuni za Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD.

Kanuni ya 18 (1) inasema: “Malalamiko yoyote kuhusiana na mchezo yawasilishwe kwa maandishi kwa kamishna wa mchezo au TFF sio zaidi ya masaa sabini na mbili (72hrs) baada ya kumalizika mchezo.”

Kanuni ya 18 (2) inasema: Ada ya malalamiko ni shilingi laki tatu (Tshs 300,000.00). Malalamiko yo yote yatakayo wasilishwa bila kulipiwa ada na kuwasilishwa nje ya muda uliowekwa hayatasikilizwa.”

Hata hivyo, Shirikisho linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kadi nyekundu aliyopewa Mchezaji Novalty Lufunga katika mashindano ya Azam Sports Federation Cup 2016/2017.

Kwa utaratibu wa mashindano haya ambayo ni ya mtoano, adhabu za kadi (njano na nyekundu) zitolewazo uwanjani, zinakoma mwisho wa msimu wa shindano husika isipokuwa kadi hizo zikiongezwa adhabu ya kinidhamu (suspension) ambayo itafahamisha kwa klabu na mchezaji kwa maandishi.

Kadhalika, Kanuni ya 16 ya Kanuni za Kombe la Shirikisho Sehemu ya Tatu inaeleza wazi kuwa matumizi ya kanuni za ligi zitahusika maeneo yanayoruhusu uendeshaji wa shindano la mtoano.

“Adhabu zote zinazohusisha katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam HD zitahusisha na shindano hili tu,” inasema kanuni ya 16 (3) na (4).

Kambi Ya Kilimanjaro Warriors
Video: Serikali kufufua viwanda vyote vya chai