Mshambuliaji wa majogoo wa jiji Liverpool Sadio Mane ataendelea kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu, baada ya rufaa ya kupinga kadi nyekundi aliyoonyesha mwishoni mwa juma lililopita, kuwekwa kapuni na chama cha soka nchini England (FA).

Mane alionyeshwa kadi hiyo baada ya kumpiga teke la uso mlinda mlango wa Man city Ederson, katika mchezo wa ligi ya nchini England ambao ulimalizika kwa Liverpool kukubali kufungwa mabao matano kwa sifuri kwenye uwanja wa Etihad.

FA wamejiridhisha kwa kurejea picha za video za mchezo huo, na kubaini mwamuzi Jon Moss alichukua maamuzi sahihi ya kuuadhibu mshambuliaji huyo kutoka nchini Senegal, kutokana na kosa alilolifanya.

Hata hivyo meneja wa Liverpool Jurgen Klopp bado ameendelea kupingana na maamuzi hayo, kwa kusema Mane hakukusudia kumuumiza Ederson, bali kitendo kilichotokea kilikua bahati mbaya.

Kwa mantiki hiyo Mane atakosa mchezo dhidi ya Burnley utakaochezwa mwishoni mwa juma hili. Pia atakosa michezo miwili dhidi ya Leicester City ya kombe la ligi na ligi ya England.

Messi aweka rekodi mpya
Video: Wadau wa haki za binadamu walaani kushambuliwa kwa Lissu