Serikali ya Greenland katika sekta ya Afya imejichimbia kaburi kwenye suala la uzazi wa mpango na sheria ya utoaji mimba kwa wanawake.

Katika kisiwa hicho kikubwa duniani chenye idadi ndogo ya watu, wanawake zaidi ya nusu wanaopata ujauzito huwa wanatoa mimba na kupelekea idadi ya mimba zinazotolewa kuwa 30 kwa kila wanawake 1000.

Kwa mujibu wa takwimu za Serikali ya nchi hiyo, tangu mwaka 2013 watoto 700 wanaziliwa kila mwaka huku mimba 800 zinatolewa kila mwaka hivyo kupelekea idadi ya wanaozaa kuwa chache kuliko ya wanaotoa mimba na takwimu za hivi karibuni zinasema kuwa Greenland ina idadi ya watu 55,992 pekee.

Msichana wa miaka 19 aliyetoa mimba mara tano ndani ya miaka miwili alipoongea na mwandishi wa BBC, amesema huwa hafikirii mara mbili kutoa mimba anapoipata kwani jamii yake inaona ni jambo la kawaida.

“Huwa sifikirii mara mbili kuhusu jambo hili, huwa tunazungumza kwa uwazi kabisa kuhusu utoaji mimba, ninakumbuka jinsi nilivyokuwa nawaambia marafiki zangu na familia yangu mimba ya mwisho niliyotoa” ameongea Pia na kuongeza njia za kujikinga anazozitumia.

“Huwa ninatumia kinga kila mara lakini wakati mwingine huwa tunasahau. siwezi kuwa na mtoto kwa sasa nipo mwaka wangu wa mwisho wa masomo”

Licha ya kuwa Serikali ya Greenland imeruhusu utoaji mimba na unafanyika bure kwa anayehitaji lakini madhara yake yameanza kuonekana makubwa naimeshauriwa kuweka gharama kwa kila mimba itakayotolewa ili idadi ya wanaotoa mimba ipungue.

Baadhi ya wanaharakati wamekosoa vikali ushauri huo kwa kusema kuwa wanawake kutoa mimba mara kwa mara haina uhusiano wowote kuwa kutoa mimba ni rahisi na bure.

“Ninapingana kabisa na uamuzi huo maana wanaweza kwenda kutafuta sehemu ambayo wanaweza kutoa mimba kwa gharama nafuu, jambo ambalo ni hatari” mtaalamu wa afya pia ametoa msimamo wake juu ya kuweka gharama kwenye huduma ya utotaji mimba kisiwani Greenland.

Jambo lakustaajabisha ni kwamba watafiti wamebaini kuwa wanafunzi katika mji mkuu wa Nuuk huwa wanaenda kiliniki kila jumatano na huwa wanaiita siku hiyo kama siku ya kutoa mimba, mtafiti Dr.Turi Hermannsdottir amewaambia BBC.

Kutokana na ruhusa hiyo ya kutoa mimba bure Greenland imetengeneza familia nyingi zilizo na wanawake waliotoa mimba na wazazi, mwanafunzi mmoja amethibitisha hilo.

“Rafiki zangu wengi waliwahi kutoa mimba, Mama yangu aliwahi kutoa mimba tatu kabla hajanizaa mimi na kakayangu ingawa hazungumzii”

Licha ya kuwa dawa za uzazi wa mpango zinatolewa bure kisiwani humo Dk.Stine Brenoe mtaalamu wa afya ya uzazi aliyefanya utafiti kwa muda mrefu amesema kuwa karibu asilimia 50 ya wanawake ambao amewahoji wanaufahamu juu ya dawa hizo lakini zaidi ya asilimia 85 hawazitumii kwa usahihi au hawazitumii kabisa.

Hali ngumu ya kiuchumi, makazi duni pamoja na ukosefu wa elimu vimetajwa kuchangia utoaji mimba kwa kiasi kikubwa huku matumizi ya pombe yakichangia wanawake kupata mimba zisizotarajiwa na wanishia kuzitoa.

Kitendawili cha nini kifanyike kupunguza idadi ya wanawake wanaotoa mimba kisiwani Greenland bado hakijapata mteguaji hasa wakati huu ambapo jamii inapoona mimba ni kama kuumwa kichwa na kutoa ni kama kunywa dawa ya kutuliza maumivu, Serikali kisiwani humo inamtihani mkubwa wa kubadili fikira za watuwake juu ya madhara ya utoaji mimba.

Majaliwa atoa onyo kwa wamiliki wa vituo vya watoto yatima
Video: Mwanamke mwenye misuli zaidi duniani