Waziri wa Ardhi, William Lukuvi amesema wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa sheria inaruhusu majina zaidi ya mawili kusainiwa katika hati moja.

Lukuvi ametoa ufafanuzi huo jana  Desemba 19, 2020 akibainisha kuwa kufanya hivyo kunapunguza migogoro isiyo ya lazima kwenye familia wakati mmoja anapofariki dunia hasa katika masuala ya mirathi.

“Wizara ya ardhi kwa sasa inasajili majina zaidi ya mmoja kwenye hati na wale ambao wako tayari kusajili majina zaidi ya moja tunasajili yote kwenye hati na walio wengi sasa hivi wamejitokeza ili kuepusha kesi nyingi za mirathi baadaye.”

“Sasa hivi ni fursa kwa akina mama wakati wa kuandika hati washawishini waume zenu kuwe na majina yenu yote mawili ya baba na mama sheria iko wazo sisi ukija na jina moja tunasajili na hata zaidi ya moja tunasajili,” amesema Lukuvi.

Aidha Lukuvi amesema kuw ahata mototo mdogo anaweza kusajiliwa katika hati kwa masharti kuandikwa pia na jina la msimamizi.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 20, 2020
Mume, mke wahukumiwa jela miaka 20 kwa kusafirisha dawa za kulevya