Wizara ya Maliasili na utalii  kupitia Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA) imetangaza rasmi kuanzishwa kwa bucha za kuuzia nyamapori katika mikoa 23 ya Tanzania Bara.

Hatua hiyo imekuja kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Magufuli aliyoyatoa mwanzoni mwa mwaka huu wakati alipokuwa katika ziara mkoani Rukwa.

Katika ziara hiyo Magufuli alielekeza wananchi wapewe fursa ya kuifadhi Rasilimali za wanyamapori kwa utaratibu maalumu ikiwemo kuanzisha bucha za kuuzia Nyamapori.

Akizungumza akiwa mkoani Morogoro ,katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Dokta Aloyce K .Nzuki amesema hafla ya uzinduzi wa kuanzisha bucha kwa ajili ya kuuzia nyamapori ni kuekelezaji wa maelekezo ya Rais Magufuli.

Akizungumza katika hafla hiyo Dokta Nzuki amesema mikoa 23 itaanza kufaidi rasilimali hizo kwa kuanzisha bucha huku mikoa mitatu ya Songwe ,Rukwa na pamoja na Mara kutoanza utaratibu huo hadi hapo changamoto ya usimamizi wa utekelezaji wa shughuli hii itakapopatiwa ufumbuzi.

Mikoa itakayo anzishwa bucha za nyamapori ni Morogoro, Tanga, Pwani, Singida, Dodoma, Tabora, Katavi, Kigoma, Shinyanga, Geita , Kagera, Mwanza, Simiyu, Iringa, Mbeya, Njombe, Lindi , Mtwara, Ruvuma, Manyara, Arusha, na Kilimanjaro na Dar es Salaam.

Watanzania wanaotaka kuendesha biashara hiyo wanatakiwa kuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi ,uthibitisho wa maombi ya leseni pamoja na mpango wa biashara

Nyumba za ibada zisitumike kunadi sera
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 26, 2020

Comments

comments