Wahamiaji haramu sita, Raia wa Ethiopia wamekamatwa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoa wa Rukwa. Aidha Raia 18 wa Zambia na Watanzania 10 wamekamatwa kutokana na operesheni maalumu iliyofanywa na maofisa wa uhamiaji.
Mahakama hiyo pia imewatia hatiani Watanzania 10 na kuwahukumu kifungo cha mwaka mmoja, kila mmoja wao au kulipa faini ya Sh 500,000 kwa makosa ya kuwahifadhi na kuwaoa wahamiaji haramu.
Kati yao, raia 7 wa Zambia wamehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kalambo kutumikia kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 500,000 kila mmoja kwa makosa ya kuingia na kuishi nchini kinyume cha utaratibu.
Mmiliki wa Shule mbaroni kugomea agizo la Rais ”Shule zote zifungwe”
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Rukwa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Elizeus Mushongi alisema wahamiaji haramu Raia wa Zambia wengi wao walikuwa wameolewa na Watanzania na kuishi bila kufuata utaratibu.