Kocha wa Mabingwa wa Soka Afrika Kusini Mamelodi Sundowns Rulani Mokwena amesema Benchi lake la Ufundi linafahamu vyema mabadiliko yote ya kiufundi yaliyofanywa na Kocha Mkuu mpya wa mabingwa wa Soka Barani Afrika Wydad Casablanca Sven Vandenbroeck, kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Nusu Fainali, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika utakaopigwa Uwanja wa Mohammed V mjini Casablanca leo Jumamosi (Mei 13).

Kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji alitangazwa kushika hatamu ya kuliongoza Benchi la Ufundi la Wydad Casablanca juma lililopita akichukua nafasi ya Juan Carlos Garrido aliyeondoka klabuni hapo.

Hadi sasa Vandenbroeck amesimamia mechi moja akiwa na Wydad ya ushindi wa mabao 3-1dhidi ya Chabab Mohammedia.

Akiwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa leo Jumamosi Kocha Mokwena amesema: “Tumetumia muda mwingi kufanya uchambuzi wa video ili kufanya kile tunachotaka kukifanya kwa wapinzani wetu”

“Tunajua Wana Kocha mpya, lakini  timu yao haijabadilika sana, ni kama ilivyokuwa hapo awali, ina wachezaji wazuri sana, wana uchezaji wao wa mawinga wakali sana, lakini pia Wana uwezo mzuri kwenye mashambulizi ya haraka”

“Pia tulifanya kazi ya kumfuatilia vizuri kocha wao mpya (Vandenbroeck), tulipitia kazi zake katika vilabu mbalimbali nchini Saudi Arabia na Tanzania kwa undani sana” “Hii ni kazi ambayo tuliifanya siku nyingi, tukiungwa mkono sana na wachambuzi wetu. Ni kocha mzuri sana”

Rais Samia ataka gharama nafuu za Mawasiliano
Maridhiano na Serikali: CHADEMA, Lissu watofautiana