Beki wa timu ya taifa ya Tanzania ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ‘Tanzanite Queens’ Fumukazi Ally amefungiwa kucheza mitatu ya Michuano ya CECAFA inayoendelea nchini Uganda.

Fukumazi amekumbwa na adhabu hiyo, baada ya kukutwa na hatia za kumfanyia vurugu mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Ethiopia uliopigwa juzi Jumatano (Novemba 03) Tanzanite wakipigwa 2-1.

Katika mchezo huo Fumukazi alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
CECAFA pia imefungia mchezo mmoja mtunza vifaa wa ‘Tanzanite Queens’ (Kit Manager) Ester Fred Chabruma kwa kukutwa na hatia ya kumzonga mwamuzi msaidizi namba moja.

Emiliana Isaya na mwenzake Mwamvua Seif Haruna wameonywa kwa kuhusika kwao kwa asilimia kubwa kwenye vurugu hizo.

Sababu za vurugu hizo ni Tanzanite Queens kupinga maamuzi ya bao lao kukataliwa baada ya kibendera kutoa ishara ya kuwa Aisha Masaka aliyefunga bao hilo alikuwa ameotea.

Tanzanite Queens itarejea tena dimbani kesho Jumamosi (Novemba 06) kuwakabili wenyeji timu ya taifa ya Uganda, saa kumi jioni.

Majaliwa: Rais Samia ana matumaini na Taifa Stars
Taifa Stars yatengewa Bilioni 1.6