Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHAUMA , Hashim Spunda Rungwe amesema kuwa endapo atafanikiwa kuingia madarakani ataongoza kwa kufuata sheria na haki kwa wananchi .

Rungwe amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama chake eneo la Manzese jijini Dar Es Salaam.

“Mimi nikingia madarakani nitaendesha serikali ya kiraia yenye haki ya kila mtu na hakuna kuonea watu, tunataka utawala sheria kila mtu alindwe na sheria , simnanijua mimi ni wakili nitatenda haki,” amesema Rungwe .

katika hatua nyingine mgombea huyo ambae amejizolea umaarufu kwa sera yake ya ubwabwa ameitupia lawama Taasisi ya kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), kwa kuzuia asipeleke ubwabwa katika mikutano yake ya kampeni .

“tulikuwa tumepanga kununua chakula kuja hapa kwenye mkutano ,watu wa TAKUKURU wamekataza ,wamepiga mkwara kosa letu nini ?,”

Rungwe anatarajia kuendelea na kampeni kesho septemba 6 katika eneo la Kigamboni Jijini Dar Es Salaam .

Magufuli atoa ahadi nzito Mara
Barbara CEO mpya Simba SC