Klabu ya Singida Fountain Gate usiku wa kuamkia jana imemshusha nchini mshambuliaji wao mpya Elvis Rupia aliyesajiliwa akitokea Polisi PC inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya.

Rupia ambaye ni mfungaji bora wa Ligi ya Kenya msimu uliopita akiwa ametupia mabao 27, anatua kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Ghana, Bright Adjei ambaye amerejea kwa mkopo Aduana Stars ya Ghana.

Afisa Habari wa Singida, Hussein Masanza amesema kuwa usajili huosi mpya kama unavyoonekana kwani walishakamilisha kila kitu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Agosti 31, mwaka huu, isipokuwa mshambuliaji huyo alichelewa kutokana na majukumu ya timu yake ya taifa.

“Rupia hatukumsajili jana wala juzi, alisajiliwa kabla ya dirisha halijafungwa isipokuwa hii ndio mara ya kwanza anakuja Tanzania sababu alikuwa na majukumu mengine ya timu ya taifa ndio maana amechelewa, alisema Masanza.

Alifafanua kuwa mchezaji huyo atatumika kwenye michuano yote watakayoshiriki, japokuwa atakosekana kwenye mchezo wao wa keshokutwa Jumapili (Septemba 17) hii wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Future FC ya Misri kutokana na kuchelewa kujiunga na kikosi hicho kilicho chiní ya Ernst Middendorp.

Chilambo amuhofia Djuma Shaban Azam FC
Gamondi: Pengo la Mwamnyeto linazibika