Askari wanne wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wamefukuzwa kazi na maofisa wawili wa jeshi hilo wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh100 milioni.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo ametoa taarifa hiyo leo Alhamisi Aprili 29 ,2021 na kubainisha kuwa siku ya Aprili 19, 2021 walipokea taarifa kuhusu askari hao kwamba wameomba na kupokea rushwa na uchunguzi ukaanza.

“Baada ya uchunguzi jeshi limewafukuza kazi askari wanne na kuwasimamisha kazi maofisa wawili kwa kuwa haliwezi kuvumilia tuhuma hizi,” amesema Kamanda Masejo.

Amebainisha kuwa baada ya uamuzi huo hatua nyingine za kisheria zinafanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Waziri Mkenda awaonya jeshi la polisi
Polepole: Wajumbe kutoka sehemu mbalimbali watashiriki