Wizi wa kiasi cha shilingi bilioni 6.3 umebainika nchini Kenya baada ya kufanyika kwa manunuzi ya mahindi huku kiasi kingine cha shilingi bilioni 1.9 kikibainika kuibiwa katika uuzaji wa mbolea kwa wakulima.
Hayo yamebainishwa na mchambuzi wa masuala ya siasa nchini humo, Chekai Mussa alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa DW ambapo ameeleza jinsi fedha hizo zilivyochotwa.
Mussa amesema kuwa wakati wa kilimo wakulima wamekuwa wakiuziwa mbolea kutoka serikalini kwa bei ya juu zaidi huku akitolea mfano sehemu ambayo anatoka yeye katika ukanda wa bonde la ufa.
Aidha, amesema wakati wa mavuno serikali ya nchi hiyo imekuwa ikinunua mahindi kwa wakulima kwa bei ya chini zaidi hivyo kuwafanya wakulima wa mahindi kukosa faida yeyote.
Amesema kuwa kumekuwa na wakulima hewa ambao wamekuwa wakifanya biashara ambapo wamekuwa wakifoji nyaraka hewa ambazo zimekuwa zikilipwa kwa watu hewa.
-
Rais wa Ghana amsweka ndani Mwenyekiti wa Shirikisho la Kandanda
-
Mkuu wa Jeshi la Polisi awaamuru wananchi kuwapiga mawe Polisi
-
Masharti magumu yaliponza Kanisa, sasa kuburuzwa Mahakamani
Hata hivyo, ameongeza kuwa tume za uchunguzi ambazo zimekuwa zikiundwa na serikali hiyo hazina msaada wowte kwani hazitoi matokeo ya chunguzi zinazofanyika.