Marekani na Urusi zimekubaliana mpango unaolenga kumaliza vita nchini Syria na kuanza mchakato wa mpito wa kisiasa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, amesema mpango huo utahusisha usitishwaji wa mapigano kwa kipindi cha siku saba mfululizo kote nchini Syria, kuanzia jumatatu ijayo.

Kerry amesema mpango huo unatoa mwelekeo bora zaidi kuliko mapendekezo mengine ambayo yalishawahi kutolewa, na iwapo utatekelezwa na pande zote mbili, basi utatoa nafasi ya majadiliano kuhusu mustakabali wa kisiasa nchini Syria.

Aidha John Kerry aliongeza kuwa baadhi ya mambo muhimu katika mpango huo ni kwamba vikosi vya serikali ya Syria havitaruhusiwa kuendesha oparesheni za angani katika maeneo ya waasi wa upinzani wanaoungwa mkono na serikali ya Marekani.

Vikosi vya serikali na upinzani vitahitajika kufungua barabara zinazoelekea mji uliozingirwa wa Allepo, na kwamba mashirika ya msaada yaruhusiwe kuingia mjini humo bila kudhibitiwa

Kwa upande wake Waziri wa mambo ya nje wa Urusi , Sergei Lavrov, amesema mpango huo ni muhimu na halisi, na kuongeza kwamba tayari, Rais wa Syria Bashar al assad ameshapewa taarifa kuhusu mpango huo, na kutakiwa kuunga mkono, Kerry pia amesema kwamba iwapo vita itapunguwa kwa kipindi kirefu kote nchini Syria, basi Urusi na Marekani watashirikiana kuvamia Islamic State na kundi la Nusra Front

Video: DC Mjema akifungua shindano la MIss Ilala 2016
Umoja wa Mataifa Kuiwekea Korea Kaskazini Vikwazo