Katika usajili wa dirisha dogo, klabu ya Ruvu Shooting imesajili wachezaji watano vijana ili kukiongezea nguvu kikosi katika duru ya lala salama ya Ligi kuu ya Voda com Tanzania bara 2017/18.
Wachezaji waliosaini mkataba kutumika katika kikosi cha Ruvu Shooting ni kiungo namba nane Hamis Salehe Maulid na Adam Ibrahim Abdallah ambaye ni winga wa kulia.
Wengine ni washambuliaji Gidion Brown Benson na Alinanuswe Martin Mwaisemba na beki Rajab Zahir Mohamed.
Wachezaji hao tayari wako kambini wakiendelea na mazoezi isipokuwa Zahir ambaye ataripoti kambini muda wowote kuanzia sasa.