Fainali za nne za mataifa bingwa barani Afrika (CHAN 2016), zinatarajiwa kuanza kesho mjini Kigali nchini Rwanda kwa kushuhudia miamba 16 iliyowekwa kwenye makundi manne tofauti ikipapatuana.

Michuano ya CHAN ambayo inashirikisha wachezaji wanaocheza katika ligi za barani Afrika, kwa mwaka huu zinatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na utayari wa timu shiriki ambao umeonekana katika harakati za maandalizi.

Nchi ya Rwanda imeonyesha kujiandaa kikamilifu kwa kutayarisha viwanja vinne ambavyo vitatumika kwenye michuano hiyo, huku uwanja mkubwa miongoni mwa viwanja hivyo ni ule wa Amahoro uliopo mjini Kigali, ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 30,000 walioketi.

Viwanja vingine ni Huye uliopo katika mji wa Butare, ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000 walioketi, Regional Nyamirambo uliopo mjini Kigali wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 22,000, pia uwanja mwingine utakaotumika katika michuano hiyo ni Umuganda uliopo Gisenyi ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 5,000.

Wenyeji Rwanda wamepangwa katika kundi A, ambalo linatimu za Gabon, Morocco, Ivory Coast watatumia viwanja vya Amahoro na Stade Huye.

Kundi B lina timu za DR Congo, Angola, Cameroon na Ethiopia timu hizi zitatumia viwanja vya Amahoro na ule wa Stade Huye.

Katika kundi C kuna timu za Tunisia, Nigeria, Niger na Guinea timu hizi zitachuana katika viwanja vya Regional Nyamirambo na ule wa Umuganda.

Zimbabwe Mali Uganda pamoja na Zambia wapo kwenye kundi D, na watatumia viwanja vya Umuganda na Regional.

Michuano hii itafikia tamati Februari 7 kwa mchezo wa fainali itakaopigwa kwenye dimba la Amahoro Jijini Kigali.

Heather Watson Atupwa Nje Hobart
Andy Carroll Aendelea Kukumbwa Na Majanga