Makadirio ya umri wa kuishi kwa wakazi wa nchi za Afrika Mashariki (EAC) unatarajiwa kukua na kufikia wastani wa miaka 75 ifikapo mwaka 2040.
Lakini nchi ya Rwanda kwa sasa inaongoza ikiwa na umri wa wastani wa miaka 67.8 na inatarajiwa kukua na kufika miaka 77.6. nchi ya Kenya ndio inayo fuatia ambayo wastani wa watu wake kuishi ni miaka 66.9 huku ikitarajiwa kukua haidi miaka 73.5 ifikapo mwaka 2040.
Alipokuwa akitangaza takwimu hizo jijini Washington, Marekani Mkurugenzi wa takwimu katika taasisi ya Afya na tafiti, Dk Kyle Foreman, ameitaja Tanzania kuwa wastani wa umri wa watu kuishi kwa sasa ni miaka 64.3 na inatarajiwa kufia miaka 72.3 kwa mikakati ya sasa iliyojiwekea na ikiboreshwa zaidi itafikia miaka 75.9. huku Uganda ikiwa na wastani wa umri wa kuishi miaka 62.2.
kwa takwimu hizo licha ya Tanzania kuwa nafasi ya chini, umri wa kuishi umeongezeka kutoka miaka 37 mwaka 1978 hadi kufikia miaka 65 mwaka 2018, ripoti hiyo pia inaonesha idadi ya watu imefikia milioni 54.2 mwaka huu na inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2021 itafika milioni 59.
Na katika utafiti huo unaonyesha kuwa changamoto kubwa inayopunguza umri wa watu kuishi Afrika ni magonjwa yasiyoambukizwa na yanatarajiwa kuwa sababu kubwa ya vifo vya watu katika nchi za Afrika Mashariki ifikapo 2040, yakiwemo kisukari, figo, saratani za aina mbalimbali na uzito ulio kithiri.