Raia wa Rwanda wanaombolezo vifo vya watu zaidi ya 130, waliofariki kutokana na mafuriko yaliyokumba eneo la magharibi mwa nchi hiyo na mamia ya nyumba kuharibiwa.
Maombolezo hayo, yanafanyika wakati huu Serikali ikiendelea kukadiria hasara iliyotokana na mafuriko, huku shughuli za mazishi pia zikiendelea kufuatia majanga hayo mabaya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo.
Baadhi ya familia zimeeleza namna zilivyopoteza ndugu zao, baada ya kufukiwa na vifusi vya udongo na kuta za nyumba huku wengine wakisema shughuli za maisha ya kawaida zimekoma rasmi baada ya kupoteza mali nyingi ambazo walikuwa wakizitegemea kukimu familia.
Tangu Mei 2, 2023 maeneo ya kaskazini, magharibi na kusini mwa Rwanda, yameshuhudiwa kuwa na mafuriko yaliyosababisha maafa kwa raia, huku miongoni mwa waliofariki wakiwemo wanafunzi 15 na shule 33 kuharibiwa.