Wakuu wa polisi wa nchi za Rwanda na Benin, wamekutana na kujadili njia za kuimarisha ushirikiano na kuunga mkono nchi hiyo ya Afrika Magharibi za kutafuta usaidizi wa kijeshi ili kukabiliana na hali mbaya ya uasi wa kigaidi.

Mazungumzo hayo, yamefanyika kati ya wakuu hao wawili Inspekta Jenerali wa Polisi wa Rwanda (IGP), Dan Munyuza na Mkurugenzi Mkuu wa Polisi wa Jamhuri ya Benin, Soumaila Allabi Yaya mjini Kigali wakishirikisha wajumbe walioambata nao.

Msemaji wa Polisi wa Kitaifa wa Rwanda, Apollo Sendahangarwa amesema, “Kigali inaweza kutoa msaada wa vifaa lakini haitahusisha kupeleka wanajeshi wa Rwanda nchini humo ikiwa kuna mipango ya kupelekwa nchini Beni,” ambapo mazungumzo hayo hayakuhusisha mikataba iliyotiwa saini.

Wanajeshi wa Rwanda na Mgeni wao kutoka nchini Benin. Picha na IGIHE.

Akiongea katika maungumzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Polisi wa Benin, Soumaila Yaya amesema “Ninajua Rwanda mna mbinu nyingi katika vita dhidi ya ugaidi, na tunataka kujifunza kwenu ili kulinda nchi yetu, ambayo imekuwa ikikumbwa na maandamano machafu ya watu wasiotii sheria.”

Benin, pamoja na mataifa ya Ghuba ya Guinea ya Togo na Cote d’Ivoire, yameshuhudia kuongezeka kwa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wanaohusishwa na al Qaeda na Islamic State, huku ghasia zikitanda kusini kutoka nchi za Sahel za Mali, Burkina Faso na Niger.

Ujumbe huo wa Benin, uko nchini Rwanda kwa siku tano ili kujifunza na kupata msukumo wa uzoefu wa kulinda amani wa Rwanda, huku nchi zote mbili zikijaribu kuimarisha ushirikiano wa kiusalama, ikiwa ni pamoja na mapigano ya kiuhalifu.

Azam FC waanza safari ya kurudi Chamazi-Dar
Kocha Nabi atofautiana na Mashabiki Young Africans