Rwanda na Jumuiya za Kimataifa, hii leo Aprili 7, 2023 wameadhimisha kumbukumbu ya miaka 29 ya mauaji ya Kimbari yaliyotukia mwaka 1994 ambapo Wahutu wenye msimamo mkali waliwaua watu karibu milioni moja wengi wao wakiwa ni Watutsi.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza April 7 mwaka 1994 na vilivyodumu kwa siku 100, vilishuhudiwa siku moja tu baada ya kudunguliwa kwa ndege aliyokuwamo rais wa wakati huyo wa Rwanda Juvénal Habyarimana pamoja na yule wa Burundi Cyprien Ntaryamira.

Viongozi hao walikuwa wametoka kwenye mkutano wa kilele nchini Tanzania ambako walikuwa wanajadili mzozo huo wa Rwanda na aauji hayo ya kimbari ya mwaka 1994 ni miongoni mwa matukio mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Rwanda.

Rais wa Rwanda, Kagame amewasha mwenge katika makumbusho ya kitaifa ya Kigali, ambapo unatarajia kuwaka kwa siku 100, huku tofauti na miaka mingine kwa mwaka huu hakutakuwa na maadhimisho ya kitaifa.

Meridianbet yaja na Sloti yenye Ushindi Rahisi
Wafanyabiashara waonywa ununuzi mifugo ya wizi