Wizara ya Afya nchini Rwanda imewahakikishia wananchi wake kuwa serikali imejitayarisha vilivyo na iko tayari kuzuia uwezekano wowote wa kuzuka maambukizi ya Ebola.
Imesema kuwa tayari ukaguzi wa wasafiri wanaoingia nchini humo umekuwa ukifanyika, kufuatia kuzuka kwa mlipuko wa ugonjwa huo nchini DRC.
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa lengo kubwa ka kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa dalili yeyote ya kuzuka kwa Ebola inazibitiwa na kutambuliwa kwa haraka zaidi.
Vilevile imeongeza kuwa wasafiri au wageni wanaoingia nchini humo hupimwa joto la mwili na kuulizwa historia ya safari walizofunga, na pia huchunguzwa kwa dalili nyingine zozote za homa hiyo inayotokana na virusi vya Ebola.
Hata hivyo, kwa sasa tahadhari imetolewa kwa wananchi kutosafiri kwenda katika maeneo yaliyo athirika na kuripoti dalili zozote wanazohisi.
-
Afisa usalama wa taifa Kenya akamatwa na ‘unga’
-
Kim K ashtushwa na jibu la Kanye West kwa Rais Museveni
-
Mwanafunzi aua wenzake 19 kwa risasi, ajiua