Rwanda imetangaza kuwa Mgonjwa huyo raia wa India aliyeingia nchini humo Machi 08, 2020 akitokea Mumbai, India alikuwa na dalili za Corona na aliripoti Kituo cha Afya Machi 13.
Rwanda inakuwa Nchi ya 2 kwa Afrika Mashariki na ya 20 kwa Afrika kutangaza Mgonjwa wa Corona. Kenya ambayo ipo Afrika Mashariki ilitangaza Mgonjwa wake wa kwanza jana.
Nchi nyingine za Afrika ni Morocco, Tunisia, Egypt, Algeria, Senegal, Togo, Cameroon, Burkina Faso, Democratic Republic of Congo, South Africa, Nigeria, Ivory Coast, Gabon, Ghana, Guinea, Sudan, Ethiopia na Mauritania.
Shirika la afya duniani WHO linasema wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu kama Shinikizo la Damu, Kisukari, Matatizo ya Figo ndiyo walio kwenye hatari zaidi ya kuathika pindi wanapopatwa na virusi vya Corona. Watu wa umri wa wastani na wenye afya imara wanaweza kupata virusi vya Corona na kupona bila kuhitaji matibabu.