Aliyekua mshambuliaji wa pembeni wa majogoo wa jiji Liverpool Ryan Babel huenda akarejea kwenye klabu yake ya zamani ya Ajax Amsterdam ya nchini Uholanzi.

Babel ameonyesha dalili za kurejea tena Amsterdam ArenA, baada ya kuonekana akifanya mazoezi na kikosi cha klabu hiyo, ambacho kwa msimu huu kimedhamiria kurejesha heshima ya kuwa bingwa wa Eredivisie kufuatia kumaliza kwenye nafasi ya pili msimu uliopita.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, amelazimika kurejea nyumbani kutokana na uongozi wa iliyokua klabu yake ya Al Ain ya falme za kiarabu kuvunja mkataba na kumuacha kuwa mchezaji huru.

Kwa mara ya kwanza Babel aliondoka Ajax Amsterdam 2007 baada ya kusajiliwa na klabu ya Liverpool ya England, na alirejea tena Amsterdam ArenA mwaka 2013 akitokea nchini Ujertumani alipokua akiitumikia klabu ya 1899 Hoffenheim na baadae alielekea nchini Uturuki kujiunga na Kasımpaşa kabla ya kutimkia falme za kiarabu.

Vadim Vasilyev Azishutumu Man Utd, Chelsea
Kaseja Aitwa Timu Ya Taifa Soka La Ufukweni