Klabu ya Manchester United inatarajiwa kukamilisha dili la kumsajili kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Juventus FC ya Italia Paul Pogba ndani ya saa 48 zijazo.

Man utd wanatarajiwa kukamilisha dili hilo kwa ada ya usajili itakayovunja rekodi ya dunia, ambayo kwa sasa inashikiliwa na mshambuliaji kutoka nchini Wales na klabu ya Real Madrid, Gareth Bale.

Man Utd tayari wameshawasilisha ofa ya Pauni milion 100, huko Juvestus Stadium na baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa, uongozi wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC umeshaikubali.

Jambo lingine ambalo linaonyesha dalili za dili la usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 huenda likakamilishwa ndani ya saa 48 zijazo, ni mazungumzo ya uhamisho huo ambayo yamemuhusisha mtendaji mkuu wa  Juventus FC, Giuseppe “Beppe” Marotta na wakala wa Pogba (Mino Raiola).

Wawili hao walikua wakipingana katika suala la mgao wa fedha za wakala ambazo zinakadiriwa kufikiwa Euro milion 25, ambazo zinatakiwa kulipwa tofauti na ada ya usajili wa Paul Pogba.

Man Utd wamedhamiria kumrejesha Pogba Old Trafford, baada ya kuridhishwa na uwezo wake, lakini ikumbukwe walikubali kumuachia mwaka 2012 alipokua na umri wa miaka 19 kwa kigezo cha kutokidhi vigezo vya aliyekua meneja kwa wakati huo (Sir Alex Ferguson).

Kama mipango itakwenda kwa namna inavyotarajiwa, Pogba atasaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia Man Utd, na mshahara wake wa kila juma utakua Pauni 250,000.

Justin Bieber apiga chini dili nono la filamu, akataa kuigiza kama ‘Shoga’
Chelsea Waichapa Liverpool, Fabregas Aonyeshwa Nyekundu